Siku moja nikiwa nimekaa na marafiki zangu tukiwa tunabadilishana mawazo mara ghafla nilimuona mdogo wang akikimbia kwa kasi sana kuja pale tulipokuwa na marafiki zangu na alipofika ghafla akasema
Mdogo wanu: Kaka mama
Mimi: Kuna nini mdogo wangu?
Mdogo: mama yupo kule
Mimi: wapi hebu sema haraka maana sikuelewi?
Kwa hakika mdogo wangu alishindwa kusema ni nini kilichotokea hivyo tukatoka pale moja kwa moja na marafiki zangu tukiwa tunamfuata mdogo wangu Ally ambaye alikuwa katangulia mbele yetu huku akilia, sikuweza kuelewa kwa maana sikuwaza kama kingetokea kilichotokea siku ile.
Tulitembea kwa muda wa dakika tano kisha tukafika nyumbani nilipokuwa nikiishi na mama yangu na mdogo wangu.
Laaaah! Sikuamini nilichokiona mbele yangu kwa maana mama alikuwa amelala yuko hoi hajitambui, ghafla nilishikwa na bumbuazi kwani nilipojaribu kuangalia mapigo ya moyo wa mama tayari yalikuwa yameshasimama .
Nilikosa nguvu na kujikuta naanza kulia kama mtoto lakini kwa wakati huo mdogo wangu alikuwa analia sana na sikupata ujasiri wa kumueleza kuwa mama ambaye kwake alikuwa ni dada yake kipenzi Tayari ameshaaga dunia nilichokifanya nilitoka nje bila kumsemesha mtu yeyote na kwenda kwa Mjomba ambaye alikuwa karibu na pale nyumbani kwetu. Nilipofika nikamkuta yupo anacheza na mtoto wake wakiwa na furaha kubwa, basi nikaona siyo vyema nikamueleza kuwa mama ameshaaga dunia. Nilitoka pale nyumbani kwa mjomba hali ya kuwa sijitambui.
Nikiwa njiani mara ghafla niliona ni kama ndoto kwa maana nilipozinduka nilijikuta nipo hospitali mguu ukiwa umevunjika na pia nilikuwa nimewekewa pamba maskioni ishara ya kuwa tayari nilikuwa mfuu.
Hivyo kutokana na kwamba nilihisi mambo yote yalikuwa ni kama ndoto nikatoka pale sehemu ambayo ilikuwa ni monchuary, basi nilitoka pale lakini baada ya kufika pale mlangoni nilianza kugonga mlango kwa maana ulikuwa umefungwa kwa nje, niligonga mlango zaidi ya maya kumi lakini hapakuwa na mafanikio yoyote.
Baada ya kuona kuwa hakuna wa kunifungulia nilibadili nguo na kuvaa nguo ambazo zilikuwa pale ndani kisha nikaelekea kwenye dirisha lilikuwa pale ndani kisha nikalifungua nilipochungulia nikamuona nesi mmoja alikuwa anasafisha madirisha ya pale kwenye mjengo.
Upande wa pili marafiki zangu waliwataarifu
majirani na watu wengine kuwa mama yangu ameshafariki dunia hivyo walianza kufanya maandalizi ya
kumfanyia mazishi mama.
Haikuwia vigumu kufanya maamuzi juu ya
kumzika mama yangu kwani katika familia
yetu tulikuwa wawili tu, mimi na mdogo wangu Ally
Wakati huo mimi nilikuwa naelekea nyumbani
sasa kujua ni kipi kinachoendelea huku kichwani nikiwa na makovu kichwani.
Nilifika nyumbani na kuwakuta watu wamekaa
huku wakilia kwani mama yangu alikuwa akiishi na majirani zake vizuri hakuwahi
kugombana na mtu yeyote katika kijiji chetu cha MANDONDE kutokana na sifa hiyo ya mama basi ilitufanya kupendwa sana
na majirani zetu hasaaa mdogo wangu Ally ambapo yeye alikwa ni mtoto mtiifu sana pale mtaani kwetu.
Dah baada ya kufika pale nyumbani watu
walishtushwa sana na ujio wangu, kwani mwili wangu ulikuwa umejaa makovu baada
ya kufika tu ghafla ukimya ulitawala na wale waliokuwa wakilia wote walinyamaza
ndipo hapo akanyanyuka mama mmoja ambaye alikuwa ni rafiki mkubwa sana na mama
yangu na kisha akanifuata nilipo na kuniuliza
Mama: Mwanangu kimekusibu nini mpaka umekuwa
kwenye hali hii.
Dah swali la mama Yule lilinifanya kudondosha
chozi kwa maana nilimkumbuka mama yangu ambaye kwa muda huo alikuwa anaandaliwa
na safari yake ya mwisho, nilianza kutiririkwa na machozi kiasi ammbacho
nilisababisha hata Yule mama nae aanze kulia.
Alikuja rafiki yangu Harry na kuniuliza kuwa ni nini
kimenitokea?
Nikamwambia wakati nilipotoka pale ndani
nilikuwa nikielekea kwa mjomba HASHIMU kumueleza juu ya kifo cha mama lakini baada ya kufika kwa
mjomba nilimkuta yuko anacheza na mwanae hivyo nikaona siyo ningefanya vibaya
kumpa taarifa ile ambayo ingeharibu furaha yake, sasa mda ule natoka kwa
mjomba baada ya kutembea hatua kadhaa
kutoka getini kwa mjomba sikujua ni nini kilichonitokea bali nilijikuta tu nipo
sehemu ya kulaza maiti.
Harry: Enheee baada ya hapo nini kikatokea?
Mimi: unh baada ya hapo nikanyanyuka na kutoa
pamba zilizokuwa maskioni na puani kisha nikavaa kuna hizi nguo ambazo zilikuwa
pale ndani lakini wakati nataka kutoka………………
Mjomba: Ahmed umekuwaje mjomba
Mimi: nimepata ajali kidogo wakati nakuja
kukupa taarifa Juu ya kifo cha mama nikiwa njiani nikagongwa na gari kisha watu
wakanipeleka hospitali, niliogopa kumueleza mjomba kuwa mimi tayari nilikuwa ni
mfu aliyefufuka nikaamua kuishia hapo.
Baada ya kumwambia vile mjomba alinishika
mkono na kwenda nae mpaka ndani ulipolazwa mwili wa marehemu mama yangu.
Kisha ukawa ni muda wa kuuga mwili wa mama
yangu na baada ya hapo ikawa ndiyo mwisho wa kumuona mama yangu.
Watu walitoka nje huku wakiwa wamebeba jeneza
ambayo ilikuwa ni usafiri wa kumsafirisha mama yangu na safari yake ya mwisho,
pembeni yangu alikuwa mdogo wangu Ally ambaye
yeye wala alikuwa haelewi ni nini kinachoendelea.
Baada ya kumzika mama yangu tulirudi nyumbani
huku nikiwa na majonzi moyoni na pia huzuni usoni.
Siku hiyo mpaka usiku watu walikuwa bado wapo
pale nyumbani wakijadili juu ya msiba wa
mama.
Siku ya kwanza ilipita watu wakazidi kupungua
siku ya pili nayo watu wakapungua tena tukabaki ndugu na majirani wa pale
karibu na nyumbani na siku ya tatu ilipofika watu walikuja wengi wengi na
kisha tukaomba dua kuanzia saa 2 asubuhi
mpaka saa 4 asubuhi baada ya hapo watu walipata sadaka ya pilau Kwa nyama, wale wa kula kwa kukomoa
nao walikula lakini pia wale wa kubeba chakula kupeleka majumbani mwao
walifanya hivyo.
Siku ya siku ilipofika nilijikuta nimebaki
mimi na mdogo wangu Ally
tu pale nyumbani.
Mchana wa siku hiyo nilikuwa nimekaa kwenye
mti karibu na nyumba yetu nilimuona mdogo wangu Ally akiingia ndani kisha baada
ya kuingia ndani akaanza kumuita marehemu mama.
Dah! Hakika iliniuma sana haraka haraka
nikashuka mtini na kuelekea alipo Ally kisha nikamuuliza unalia nini? Akasema kuwa
njaa inamuuma nikamwambia usijali twende huku.
Tulitoka pale na kuelekea kibanda walichokuwa
wanapika chakula kisha nilimuomba mhudumu ampe Ally chakula ambacho
kingemtosheleza akapewa chakula akala akashiba lna hapo wazo tena la kumtaka
mama hakuwa nalo tena..
Tulitoka pale wanapouza chakula kisha tukarudi
nyumbani tulipofika tu Ally aliingia
ndani kisha akawa amelala.
Nikiwa nimekaa pale mlangoni mara ghafla
kichwa kilianza kuuma kiasi kwamba nilihisi kichwa kinataka kupasuka na baada
ya dakika kadhaa nikaanza kuona Mawenge kiasi kwamba hata kitu kingepita mbele
yangu nisingekiona.
Baada ya muda nilirudi katika hali yangu ya
kawaida lakini dah kila niliyemuona pale mbele yangu alikuwa ni mtu mgeni
hakuna hata ambaye nilikuwa nikimjua.
Ndipo baada ya kuamka swali la kwanza
niliwauliza nipo wapi? Na je nyie ni wakina nani?
Dah swali lile kwa hakika liliwaumiza sana
wale waliokuwa pale kabla hawajasema chochote mara akaingia daktari aliyekuwa
ameshika karatasi na baada ya kufika pale akasema kuwa nimepatwa na tatizo la
kusahau kutokana na kwamba kuna uvimbe kwenye kichwa changu ambao ulisababishwa
na ajali ya siku ile..
Nilikaa pale hospitali kwa muda wa siku tatu
huku nikiwa sikumbuki kitu chochote lakini pale alipokuwa anakuja Ally nilikuwa
nikimpenda sana japo nilikuwa simkumbuki lakini nilitokea kumpenda sana bila
kujua alikuwa ni mdogo wangu.
Niliporudi nyumbani baada ya kupita siku
kadhaa nikiwa hospitali basi kuna jirani yetu ambaye alikuwa ni rafiki mkubwa
sana na mama yetu ambaye kwa hakika alimpenda sana Ally alimchukua na kuwa anakaa
nae na niliporudi japo nilikuwa sikumbuki chochote ila aliniomba kuwa akae na
Ally name kwa kuwa sikuwa nikimkumbuka nilikubali. Basi maisha yakaendelea.
MIEZI
SITA (6) BAADAE
Siku moja nilikuwa nimekaa kwenye mti ule
uliokuwa karibu na pale nyumbani basi ghafla mawazo nilijihisi wa tofauti maana
kila kitu nilianza kukikumbuka baada ya ya Ally kuja na Kuniita kwenda kula
chakula.
Nilienda
kula chakula kwa rafiki yake mama ambaye kwa mda huo nio alikuwa kama
mama yetu.
Baada ya kumaliza kula nilimwambia “hakika
mama nashukuru kwa wema wako ila naomba niseme kitu kimoja hakika wewe hauna
tofauti na mama yetu hivyo nakuomba sana nisaidie kumtunza mdogo wangu kwa
maana wewe sasa ndiye mama wa mtoto huyu
hana pengine pa kutegemea ijapokuwa kaka yake nipo lakini sina kitu na itaniwia
vigumu kumtunza mdogo wangu tafadhali mama”
Mama: “usijali mwanangu huyu sasa ni kama
mwanangu kama unavyojua kuwa mama yako sijabahatika kuwa na mtoto hivyo Ally
nitamtunza, kumpenda, na kumjali kama mtoto wangu wa kumzaa”.
Dah! kwa hakika maneno ya mama huyo yalinipa
furaha na kunifariji kiasi Fulani na kuamini kwamba mdogo wangu ataishi kwa
furaha kubwa maana hata baada ya kufa
mama nilikuwa na wasiwasi ni jinsi gani naweza kumlea mdogo wangu hali ya kuwa
sina kitu?
kisha nikamwambia “ nashukuru sana mama kwa Maneno yako mazuri na yenye faraja
lakini pia nami nitakuwa najitahidi kadri niwezavyo ili kumlea mdogo wangu.
Nilitoka pale hali ya kuwa tayari nina amani
tele moyoni.
Basi baada ya kutoka pale nilienda nyumbani
na kisha nikaanza kutafuta vyeti vyangu vya shule pamoja na chuo ili
kuhakikisha kama naweza kuvikuta kwa maana alikuwa navyo marehemu mama.
Lakini kwa bahati nzuri havikuwa mbali sana
nilivikuta na kisha nikaviweka kwenye begi langu na kingine cha Ally ambacho
kilikuwa ni cha kuzaliwa basi sikuwa na budi nilienda kumkabidhi Mama anae mlea
mdogo wangu.
Usiku uliingia na mimi nilikuwa nikijiandaa
na safari ya kuelekea mjini kwenda kutafuta kazi.
Basi nilipanda kitandani huku nikiwa
natafakari nitaenda lakini sikujali kwa maana mfukoni nilikuwa na Shilingi laki
mbili (200,000/=)
hivyo nikaamini
zingenisaidia huko nitakapoenda.
Kesho yake asubuhi na mapema nilielekea kituo cha mabasi ambacho kilikuwa
mbali kidogo na nyumbani hivyo ilinibidi kuamka mapema sana.
BAADA
YA MIEZI MITATU
Nilikuwa katika ya jiji la Mwanza nikiwa
sielewi ni njia gani nitafanya ilikupata kazi kwa maana nimejaribu kupita kila
njia kwa hakika sikuona mafanikio, na nikikumbuka ni kiasi gani rafiki yangu
ambaye tulisoma wote chuo alivyonisaidia na kunipa hifadhi hivyo nikawa na wivu wa maendeleo juu
yake nami nikatamani mda huo niwe kama yeye au nimzidi yeye hivyo kila siku
nilikuwa ni wa kupita kwenye maofisi ya watu kutafuta kazi.
Siku zilipita miezi nayo haikubaki nyuma
wakati huo nimekuwa nikimtegemea rafiki yangu Calvin ambaye ndiyo alikuwa
msaada mkubwa kwangu.
Siku nikiwa niko nyumbani nimekaa mara ghafla
simu yangu iliita na baada ya kuangalia ni Calvin alikuwa akipiga simu nikapokea:
Kisha sauti ikasikika “ samahani wewe ni
ndugu wa mmiliki wa hii simu?
Nikamwambaia ndiyo huyo ni ndugu yangu kwani
kimemkuta nini akasema ndugu yako alidondosha simu yake halafu mimi ndiye
niloiokota
Dah! Kidogo nilipumu na ndipo nikapata nafasi
ya kumuuliza kuwa ni wapi atakuwa yeye ili nikaichukue alinieleza na baada ya
kunieleza nikaenda kuichukua simu yake kisha nikawa narudi nyumba.
Wakati nikiwa narudi nyumbani mara ghafla
nilichomwa na kimti kilichokuwa ardhini ambacho kilisababisha mguu uane kutoka
damu na hivyo nikajikaza kuelekea
nyumbani nikiwa niko barabarani mara ghafla kuna gari lilipita karibu
yangu na kisha ikasimama mbele kidogo na baada ya kusimama dereva alishusha
kioo na kuntoa mkono nje ishara ya uniita. Sikujua ni nani aliyekuwa akiniita
lakini nilitembea haraka kuelekea gari lilipo nilipofika nilimkuta mama mmoja
ambaye ni jirani yetu karibu na pale ninapoishi na Calvin kisha Yule mama
akaniuliza
Mama: “mguu umefanyaje mbona unachechemea?”
Nikamwambia
kuna kimti kidogo kimenichoma tu ndio maana unaona nachechemea
Mama: ah basi panda nikupeleke mpaka nyumbani
maana hata mimi naelekea huko huko
Nilishangaa na kumuuliza kwani mama unanijua
mimi?
Akacheka kidogo kisha akasema wewe si unaishi
na Calvin? Nikamwambia ndio basi story zikaendelea huku maswali ya hapa na pale
yakiendelea mwishoni akaniuliza samahani kijana unaitwa nani? Nikamwambia kuwa mimi naitwa Ahmedy naye
akajitambulisha kama mama BINAJATI nikamwambia okay nafurahi kukufahamu lakini
mimi naomba niishie hapa maana hapa kuna sehemu nataka nipite
Mama akasema hapana bwana twende kuna dawa
pale nyumbani ukachukue angalau inaweza kukusaidia……
ITAENDELEA ………………………………..
0 Maoni