JE UNAFAHAMU SIFA ZA MPENZI AMBAYE NI BORA NA WAKUKUFAA KATIKA MAISHA YAKO?????

href="www.churukuguy.blogspot.com"
watu wengi katika jamii ya sasa hivi wanashindwa kuchagua mwenza ambaye anaweza kumfaa kwa maisha yake bali wengi wao wanaangalia maslahi kuhusu fedha na hata vitu vingine vya kifahari bila kujali kama hawataishi kwa furaha au la? Hivo kutokana na haya yote leo tumewaandalia makala ili kujifunza ni wenza wa wapenzi wa aina gani ambao wanaweza kutufaa maishani mwetu na bila hata ya kujutia uwepo wao kwetu. Je? unafahamu sifa za mpenzi ambaye ni bora na ukajifunia kuwa nae muda wote? Ungana nami mwanzo mpaka mwisho na zifuatazo ni sifa za mpenzi/mwenza ambaye anaweza kuwa bora kwa maisha yako:- 1. Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.
2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili
. 3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri.
4. Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.
5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo cha maisha yako, atakulinda daima.
6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)
7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine, hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza. 8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu. 9. Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu . 10. Atakuwa tayari kuvumilia, hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe.

Chapisha Maoni

1 Maoni