SPONSOR GINNIE: STORY YA MAPENZI: EPISODE YA 01

SPONSOR GINNIE Mwandishi: Rama Nkova Mawasiliano: +255 694 253 259 Wasambazaji: Churukuguy.blogspot.com Episode 01 Ilikuwa ni siku ya Jumamosi kwahiyo nilifanya kazi sana siku hiyo, hivyo ilipofika muda wa saa tatu Usiku nilikuwa tayari nimeshakula na kuelekea zangu chumbani kisha nikajitupa kitandani, haukupita mda nilipitiwa na usingizi nikalala fofofo. Nikiwa kwenye usingizi mzito nikawa nasikia sauti kwa mbali sana ikiwa inaita jina langu nikahisi kama ni ndoto,lakini sauti ile nilivyozidi kuisikia na ndivyo nilihisi inazidi kusogea pale nilipokuwa nimelala, lakini sikuwa nikijitambua na kuhisi kuwa ilikuwa ni ndoto tu, mara ile sauti iliyokuwa ikisikia ikatoweka ukimya ukatawala, nikaendelea kuuchapa usingizi na baada ya muda nikiwa katika usingizi mzito mara nikahisi kuna mtu ananipapasa kwenye paji langu, kwa hakika sikuwa naelewa bali nilikuja kushituka pale nilipofungua macho na kukutana na sura ya mwanamke mmoja ambaye alikuwa anaishi karibu na sehemu niliyokuwa nikiishi mimi. Uoga, hofu, joto jembamba lilianza kunitiririka huku baridi Fulani hivi likipita katika vimelea vya mwili wangu na kujikuta najikunyata kwa uoga na baridi lililokuwepo mda huo, yule mwanamke ambaye kwa jina alijulikana kama HAFSA alinambia:- Hafsa: Dee usiogope kwani najua unajiuliza ni vipi nimeingia nyumbani kwako tena bila hata ya kubisha hodi na pia unajiuliza kuwa nimepitia wapi hadi kufika hapa chumbani kwako ila siyo kwamba nimekuja kukutisha hapana ulisahau kufunga mlango wako hivyo ndio maana unaniona nipo hapa, tafadhali usinifikirie vibaya. Dee: Okay Kwani unataka nini kutoka kwangu na kwanini umekuja umevaa hivo? Hafsa akajiangalia juu mpaka chini kisha akanambia Hafsa: kwani Dee nimevaaje mbona nimevaa kawaida tu? Nikamjibu kwa hasira Nikamwambia “wewe ndio, unaona umevaa kawaida lakini yote na yote umekuja kufuata nini chumbani kwangu? Hafsa aliniangalia kwa muda kidogo kisha akasema :- Hafsa: Dee kiukweli kuna jambo nahitaji kuzungumza na wewe naomba japo unipe dakika 10 tu niongee na wewe. Dee: jambo gani hilo unakuja kunisumbua usiku wote huu? Hafsa: Dee kiukweli nimeshindwa kuvumilia hisia zangu ni mda sasa nimekuwa nikibeba mzigo wa hisia juu yako lakini hata siku moja sijawahi kukuambia naomba leo unielewe ya kuwa nateseka juu ya penzi lako nimekuwa mvumilivu kwa mda mrefu lakini leo tafadhali japo nionje ladha ya penzi lako tu nakuomba Dee. Nilipatwa na hasira sana kwani Hafsa alikuwa anajua fika nilikuwa nampenda sana Rafiki yake Cleo na yeye ndiye alikuwa kila siku akiongea na Cleo kuhusu hisia zangu, nikamwambia:- Dee: Hafsa unajua fika mimi nampenda rafiki yako Cleo lakini leo unanivunjia heshima na chumbani kwangu na khanga moja tena usiku wa manane unahitaji kipi haswa kutoka kwangu, ama kweli hakuna rafiki mwenye ndoto ya kumsaidia rafiki yake kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake. Hafsa: hapana siyo hivyo Dee kumbuka Cleo tayari ana mchumba wake sasa kwanini ukazanie mtu ambaye hana mpango na wewe? Dee: Hafsa unasema nini wewe? Cleo ana mchumba? Hafsa akakaa kimya kidogo nikamuuliza tena “ Hafsa nambie Cleo anamchumba?” Cleo akaitikia “ndiyo ana mchumba na wanatarajia kufunga ndoa ifikapo mwezi wa kumi mwaka huu”. Kiukweli baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa Hafsa nilijikuta naangukia kwenye Dimbwi la mawazo huku nikiwa na hasira, machozi yananilengalenga nikamwambia ;- “Hafsa naomba ondoka chumbani kwangu na usije rudia tena kuingia chumbani kwangu na leo iwe ni mara ya mwisho na ya kwanza kuingia chumbani kwangu naomba ondoka sasa hivi sitaki hata kukuona” Hafsa alinyanyuka na kuondoka huku akionyesha kuwa mnyonge sana, Hafsa baada ya alifunga mlango na kuondoka, nikashituka nikahisi kama ilikuwa ni ndoto ila nikanyanyuka pale kitandani ili nikahakikishe kuwa ilikuwa ni ndoto lakini nilivofika mlangoni sikuamini macho yangu kwa kile nilicho kiona.................................. USIKOSE SEHEMU YA PILI NA KAMA UNAHITAJI YA KUSIKILIZA NICHEK MESSENGER NIKUELEKEZE NICHECK WHATSAPP +255 694 253 259

Chapisha Maoni

0 Maoni