SPONSOR GINNIE: STORY YA MAPENZI: EPISODE 02

SPONSOR GINNIE Mwandishi: Rama Nkova Mawasiliano: +255 694 253 259 Wasambazaji: Churukuguy.blogspot.com Episode 02 Nilipofika pale mlangoni nilishtuka sana baada ya kuona kuwa mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, uoga ulianza kunijaa nikawa najiuliza hivi ile ilikuwa ni ndoto au ni kweli? Nilisimama pale mlangoni kwa muda kidogo nikiitafakari ndoto ile lakini sikuweza kupata majibu na baada ya muda nilirudi kitandani na kuvua viatu maana sikuwa hata nimevua viatu nilivokuja kulala. Kisha nikapanda kitandani lakini usingizi kwangu ulikuwa kama ndoto tena kwani nilikuwa naogopa sana kuwa ile ndoto ilikuwa na maana gani, Ila kama unavyojua usingizi nao haukawii hata uwe katika hali gani basi usingizi ulinichukua nikalala fofofo kiasi kwamba nakuja kuzinduka ilikuwa ni saa 02asubuhi. Niliamka kutoka pale kitandani na kutoka nje ili kuangalia hali ya hewa na mazingira ya pale nyumbani, wakati natoka sikumkuta mtu yeyote nje bali ukimya ulikuwa umetawala sana. Nilizunguka kidogo tu pale nje kisha nikarudi ndani na kukaa kwenye sofa lililokuwepo sebleni kisha nikachukua simu yangu na kuanza kuchati na rafiki yangu Black nilimuelezea kuhusu ile ndoto lakini nae alisema kuwa ni ndoto tu wala haina ukweli ndani yake. Nilikaa ndani mpaka ilipofika saa 04 asubuhi nilitoka na kuelekea bafuni kwenda kuoga, nilienda kuoga na baada ya kumaliza kuoga nikawa narudi ndani kwangu ila nilipata mshituko sana baada ya kumkuta Hafsa yupo na Cleo pale nje wakiwa wanachemsha chai huku soga ikiwa imekolea, nilinyata mdogo mdogo mpaka nikaingia ndani bila wao kujua kwani sikutaka hata kuongea nao nikiamini kuwa ndoto ile ilikuwa ni ya kweli. Nilivaa nguo kisha nikawa nikajiandaa kutoka zangu kuelekea mtaani kuzunguka zunguka kutokana na kwamba siku hiyo sikuwa na kazi yoyote nyumbani, nikawasalimia wakina Cleo na Hafsa kisha nikatokomea mtaani. Nilienda kwa rafiki yangu Harry, nikakaa sana nyumbani kwake stori za hapa na pale zikiendelea ila nilipomsimulia kuhusu ile ndoto alinambia kuwa hayo ni mambo ya kawaida tu Dee ila usikute una Jini mahaba ooh!! Nikamuuliza kwani “mtu akiwa na jinni mahaba huwa anafanyaje kwani” Harry: huwa tu wanaota ndoto wanafanya mapenzi, halafu unapokuwa unatembea unahisi tu kuna mtu yupo nyuma yako lakini hata ukiangalia huoni kitu lakini pia kuna mda unahisi kuna mtu anakuita lakini ukiangalia hakuna anayekuita Uunh nilishtuka sana baada ya Harry kuniambia maneno yale na ukiangalia mimi leo nimeota hafsa anahitaji kufanya mapenzi na mimi halafu nilipokuwa barabarani kuelekea mtaani nilikuwa nahisi kama kuna mtu yupo nyuma yangu lakini kila nikigeuka nilikuwa simuoni, niliogopa sana nikamuaga Harry na kumwambia kuwa mimi narudi maskani kuna kitu naenda kufanya akaniuliza mbona mapema nikamwambia nitakuja badae. Baada ya kutoka tu pale ndani nikatafta sehemu zilipo bodaboda kisha nikarudi maskani na kujifungia ndani. Wakati huo ni muda ya saa 09 jioni, nikaenda kitandani na kujilaza tena huku nikitafakari maneno ya harry yakijirudia mara kwa mara kichwani mwangu. Nililala mpaka saa 01 jioni kisha nikaingia jikoni kutaka kuandaa chakula, nilitafuta sana kiberiti kwa muda mrefu lakini sikukiona nikataka kuelekea mtaani kufata kiberiti lakini mara nikakiona kilikuwa chini ya meza, nikawasha jiko sasa nikawa naandaa sufuria kwa ajili ya kupika nilivomaliza nikapika chakula na baada ya muda kilikuwa tayari nikapakua kwenye sahani kisha nikaenda sebleni na kuanza kula. Baada ya kumaliza nikaendelea kukaa pale sebleni na kwa vile nyumbani kwangu hapakuwa hata na TV nikawa sina hata cha kupotezea muda bali kuchat na marafiki zangu tu kwenye simu. Muda ukaenda masaa nayo yakasonga mbele nilikaa pale sebleni mpaka 02 kisha nikatoka nje nikamkuta khaled ambaye ni jirani yangu nikakaa nae na kuanza kupiga soga za hapa na pale. Ilipofika saa 4:30 kila mtu aliingia ndani kwake, mimi baada ya kuingia nikachukua taulo na kuingia nilivua suruali na kuingia bafuni kuoga. Baada ya kurudi sasa ule muda najifuta futa maji nikahisi baridi Fulani hivi ya ajibu ambapo kwa dar siyo rahisi kuwa na baridi ya namna ile, ila sikujali nikasema labda kwa vile nimetoka kuoga sasa baada ya kumaliza kufuta maji si nigeuke kuweka nguo nilokuwa nafutia maji, mungu wangu hapo haja kubwa na ndogo vyote vilikuwa vyangu, mapigo ya moyo yakawa yanaenda mbio kama beat ya Jeje nikahisi kuwa nimemsukuma mtu aliyekuwa nyuma yangu ……………………………………… Unajua ni nani mtu huyo, basi usikose sehemu ya tatu ili kujua mtu huyo ni gani? Like, comment and share kwa ajili ya mwendelezo zaidi

Chapisha Maoni

0 Maoni